NAFASI Za Kazi Kinglion Investment Ltd
NAFASI Za Kazi Kinglion Investment Ltd
Nafasi: Financial Assistant
Kinglion Investment Ltd inatafuta kuajiri Msaidizi wa Fedha mwenye bidii, uzoefu na anayeaminika.
Maelezo ya Kazi
Hii ni nafasi ya muda wote, ya kikazi (full-time on-site) iliyopo Kibaha. Msaidizi wa Fedha atakuwa na jukumu la kushughulikia miamala ya kifedha ya kila siku ikiwemo:
-
Kushughulikia ankara (invoices),
-
Kuhifadhi kumbukumbu za kifedha,
-
Kuandaa na kutoa ripoti za kifedha.
Aidha, nafasi hii inahusisha kusaidia kazi za uhasibu, kufanya uchambuzi wa kifedha, pamoja na kusaidia mawasiliano na wadau kuhusu masuala ya kifedha.
Sifa za Mwombaji
-
Uwezo mzuri wa kuchambua taarifa (Analytical skills).
-
Angalau uzoefu wa miaka 3 katika nafasi ya kiuongozi.
-
Uzoefu wa kushughulikia ankara na kuhifadhi kumbukumbu za kifedha.
-
Uelewa mzuri kuhusu masuala ya kodi za Tanzania na yote yanayohusiana nayo.
-
Uelewa thabiti wa kanuni za Fedha na Uhasibu.
-
Uwezo bora wa mawasiliano.
-
Uwezo wa kutumia kwa ufasaha Kiingereza na Kiswahili.
-
Shahada ya Chuo Kikuu katika Fedha, Uhasibu, Utawala wa Biashara au fani inayohusiana.
-
Umakini na usahihi katika utoaji wa ripoti za kifedha.
-
Uwezo wa kufanya kazi binafsi na pia kushirikiana na timu.
-
Uzoefu wa awali katika sekta ya viwanda utapewa kipaumbele.
-
Umri uwe kati ya miaka 25 – 29.
Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Kinglion Investment Ltd
Maombi yote yatumwe kupitia: kelvin.richard@kinglioncompany.com
Tafadhali ambatanisha CV yako pamoja na barua ya maombi (Cover Letter).