MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri Mbalimbali September 2025
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri Mbalimbali September 2025
Wakurugenzi wa Halmashauri Mbalimbali Tanzania wanapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa hivi karibuni na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevalia Mavazi Nadhifu
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha Uraia,Leseni ya Udereva au Hati ya kusafiria na Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Kijiji au Mtaa.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada,Stashahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form IV and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo hili.
11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
12. Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Halmashauri ya Mji Mafinga ni baridi hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri Mbalimbali September 2025
Ili kuweza kutizama orodha ya majina tafadhari bonyeza kwenye kila linki hapo chini ya halmashauri husika;
Tags: MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri Mbalimbali