NAFASI 8 za Kazi Daqing Oilfield Construction Group
NAFASI 8 za Kazi Daqing Oilfield Construction Group
Ofisi ya Rasilimali Watu ya Daqing Oilfield Constructions Group Company Limited (DOCG) inawaalika Watanzania wote wenye sifa zilizoainishwa hapa chini na walio tayari kufanya kazi katika mradi wa Marine Storage Terminal Project (MST) uliopo Chongoleani kuwasilisha maombi yao.
Nafasi ya Kazi: Wafundi Umeme (08 Nafasi)
Sifa za Mwombaji:
-
Awe raia wa Tanzania.
-
Awe na Cheti cha VETA cha Electrical Installation / Electrical Engineering (kiwango cha chini ni Daraja I, II, au III kulingana na nafasi).
-
Cheti cha Trade Test kinachotambulika na Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
-
Diploma ya Kawaida au FTC (Full Technician Certificate) katika Electrical Engineering (inapendelewa zaidi kwa nafasi za juu lakini si lazima).
-
Uzoefu wa angalau miaka 5 katika kazi za electrical installation, maintenance na repair kwenye miradi ya viwandani au ujenzi.
-
Uwezo wa kusoma na kufasiri michoro ya umeme (electrical diagrams), blueprints na technical manuals.
-
Uelewa wa kanuni za usimikaji umeme Tanzania pamoja na viwango vya EWURA.
-
Awe na leseni halali ya EWURA ya Electrical Installation (ni sharti – bila hili maombi hayatapokelewa).
Majukumu:
-
Kufanya kazi za usimikaji, matengenezo na ukarabati wa mifumo ya umeme kwa kuzingatia viwango vya EWURA na sera za kampuni.
-
Kuhakikisha uendeshaji salama wa mifumo, vifaa na nyaya za umeme kwa mujibu wa miongozo ya OSHA Tanzania.
-
Kubaini na kurekebisha hitilafu, kasoro au changamoto za umeme kwa haraka na ufanisi.
-
Kusoma na kufasiri michoro ya umeme, blueprints na manuals.
-
Kufanya majaribio, kalibisho na ukaguzi wa mifumo ya umeme ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya kisheria.
-
Kuandaa na kutunza kumbukumbu, ripoti na rekodi sahihi za matengenezo.
-
Kushirikiana na wasimamizi na wahandisi wa mradi kuhakikisha kazi zinafanyika kwa mujibu wa ratiba.
-
Kusimika na kutunza mifumo ya usambazaji umeme, taa na mifumo ya udhibiti katika mazingira ya viwandani na ujenzi.
-
Kutekeleza kwa ukamilifu kanuni za afya, usalama na mazingira katika shughuli za kila siku.
-
Kutoa ushauri wa kiufundi na msaada kwa mafundi umeme chipukizi na wanafunzi wanaojifunza (apprentices).
Muda wa Mkataba:
Mkataba utakuwa wa muda maalumu kulingana na kazi husika.
Eneo la Kazi na Makazi:
Nafasi hizi zipo Kata ya Chongoleani, Jiji la Tanga. Kampuni ya DOCG itatoa chakula na malazi ya kambini kwa muda wote wa utekelezaji wa kazi. Ni lazima waliochaguliwa kutumia malazi haya ya kambini.
Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Daqing Oilfield Constructions Group Co. Ltd (DOCG)
Namna ya Kuomba:
-
Kwa waombaji waliopo Tanga na jamii za eneo la Chongoleani: Wasilisha maombi yako moja kwa moja kwa Ofisi ya Rasilimali Watu ya DOCG kupitia Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Chongoleani, Jiji la Tanga.
-
Kwa waombaji waliopo nje ya Jiji la Tanga: Tuma maombi kwa njia ya barua pepe kupitia anuani: tz_hr@docgi.cn
Mwisho wa kutuma maombi: tarehe 10 Septemba 2025, saa 11:30 jioni (EAT)
Barua pepe lazima iandikwe kichwa cha habari (subject) cha nafasi unayoomba.
Maelekezo Muhimu:
-
Waombaji kutoka sehemu zingine za Tanzania hawatakiwi kupitisha barua zao kwenye Ofisi ya Kata ya Chongoleani; ni wenyeji wa kata hiyo pekee wanatakiwa kufanya hivyo.
-
Maombi ni bure kabisa – usilipe fedha yoyote ili kupata kazi.
-
Wanawake wanahimizwa kuomba.